Baada ya uchunguzi wa kina kufanyika na wachunguzi wa shirikisho la soka ulimwenduni FIFA wameamua kutoa adhabu ya kuwafungia miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka aliyekuwa Rais wa soka ulimwenguni FIFA Sepp Blatter na Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya Michel Platini.Blatter na Platini wamekumbana na adhabu hiyo baada ya kukutwa na hatia ya kufanya matumizi ya fedha kinyume na taratibu. Blatteranatuhumiwa kufanya malipo ya milioni 2 zaUswiss mwaka 2011 kwenda kwa Platini kama Rais wa FIFA malipo ambayo ni kinyume na taratibu na ameshindwa kuthibitisha zilitumika kufanyia nini.Blatter mwenye umri wa miaka 79 amefungiwa miaka nane kutojihusisha na masuala ya soka sambamba na faini ya 50,000 za Uswisskutokana na kushindwa kuheshimu sheria zaFIFA, wakati Platini amepigwa faini ya 80000 zaUswiss kutokana na kuhusika katika mchakato huo.“Samahani yangu binafsi kwa FIFA na kwa mchezo wa mpira wa miguu, nitapambana kwa ajili yangu na FIFA, nafungiwa miaka nane kwa kosa lipi? Nitakutana na mwanasheria wangu kujadili kipi sahihi na kipi sio sahihi na kipi ni haki. Tutakata rufaa tena” >>> Blatter